Create Account

Need some Help?

Tunakanusha mambo yafuatayo

Service Disclaimer

ScalpKingsFx ni kampuni inayojihusisha na biashara ya kubadili fedha za kigeni mtandaoni (online Forex Trading) pamoja na kutoa mafunzo ya jinsi ya kuifanya biashara hii kwa ufasaha (Forex Training). Mafunzo yote tunayoyatoa ni kwa madhumuni ya kielimu pekee na hayapaswi kuchukuliwa kama ushauri maalum wa uwekezaji katika masoko ya fedha au kuwa mbadala wa ushauri kutoka kwa mtaalamu wako wa maswala ya kifedha na uwekezaji. Wakufunzi (mentors) wetu wamechukua hatua stahiki kuhakikisha usahihi wa mafunzo yanayotolewa lakini Hakuna mkufunzi au mshauri kutoka ScalpKingsFx atakayewajibika kwa hasara yeyote utakayoipata kutokana na matumizi yeyote ya ushauri, elimu, ama taarifa nyingine yeyote iliyomo kwenye tovuti hii. Tumia tovuti hii na mafunzo yetu huku ukichukua tahadhari zako binafsi.

Create Account

Subscribe to our newsletters

3 Days Money Back Guarantee

Risk Disclaimer

Biashara ya kuuza na kununua fedha za kigeni mtandaoni inaweza kuwa fursa ngumu lakini pia yenye faida kubwa kwa wawekezaji. Kabla ya kuamua kushiriki katika soko la Forex, unapaswa kuzingatia kwa uangalifu malengo yako ya uwekezaji katika forex, kiwango chako cha uzoefu, na kiasi unachowekeza katika biashara hii. Muhimu zaidi, usiweke pesa ambazo huwezi kumudu kupoteza kwani kuna uwezekano mkubwa sana wa kupata hasara hata kupoteza kiasi chote katika ununuzi au uuzaji wa fedha za kigeni mtandaoni. Hivyo basi wakati wowote unaposhiriki katika masoko kama haya, unashauriwa kutumia kile kiasi cha fedha ambacho upo tayari kukipoteza.

Testimonial Disclaimer

Ushuhuda unaopatikana kwenye tovuti hii sio kiwakilishi cha matokeo ya wanafunzi au wateja wetu wote, wanafunzi na wateja wetu wengine wanaweza kuwa na matokeo mabaya zaidi kuliko ya hao walioonyeshwa kwenye ushuhuda. Ikumbukwe kuwa, Mafanikio ya mwanafunzi mmoja sio ishara ya matokeo au mafanikio ya wanafunzi wote. Watu waliotajwa na kuonekana katika ushuhuda uliotumiwa hawakulipwa kunukuliwa isipokuwa ni kwa matokeo yao ya ukweli. Matokeo yanatofautiana kati ya mtu na mtu na hakuna mwanafunzi anayehakikishiwa kupata faida au mafanikio katika biashara ya Forex.

Satisfaction Disclaimers

Ikiwa baada ya kumaliza mafunzo ya forex kutoka ScalpKingsFx, na kwa hali yoyote ukagundua kuwa haujaridhishwa na elimu iliyotolewa, unaweza kuomba kurudishiwa pesa ambazo umelipa na kama umelipia darasa letu lolote la mtandaoni ama huduma zetu nyingine tunazotoa mtandaoni unaweza kuomba kurudishiwa malipo yako ndani ya kipindi cha siku tatu baada ya kufanya malipo hayo. Pia ikiwa umenunua bidhaa yoyote inayotolewa na ScalpKingsFx kama vile programu, vitabu na machapisho mengine na ikatokea hujaridhika navyo, Mteja anastahili kuomba kurudishiwa malipo yake kwa muda wa week 1 tangu alipofanya manunuzi hayo.

BOFYA HAPA Kujaza fomu ya maombi ya kurudishiwa malipo

Trading Signals Disclaimers

ScalpKings Fx imekusanya best forex traders kuhakikisha wanatoa huduma bora ya biashara ya forex ikiwemo viashiria vya biashara (Trading Signals). Japo Viashiria hivyo vya biashara (Trading signals) vinavyotolewa na team nzima ya ScalpKingsFx havina uhakika wa 100%, na signal hizi hazitakiwi kuchukuliwa kama uhakika wa wewe kupata faida. Hasara yeyote inayoweza kujitokeza kutokana na kiashiria cha biashara kilichotolewa na ScalpKingsFx na ukakitumia kufungua biashara itakuwa juu yako mwenyewe na hakuna mtu kutoka ScalpKings Fx atakayewajibika na hasara hiyo.

Oops

Who Am I?

Need this Content?

Sorry...!

Usalama wa Taarifa ZakoKama sehemu ya majukumu yetu ya kila siku tunahitaji kukusanya taarifa zako za kibinafsi ili kuhakikisha kuwa tunaweza kukidhi mahitaji yako na kuwasiliana na wewe kuhusu huduma zetu. Hivyo basi, taarifa zako ni siri yetu

1. Ni namna gani tunatunza taarifa zako?

Kulinda usiri wa taarifa zako ni muhimu kwetu, ikiwa umewasiliana nasi kwa simu, kwa barua pepe, kwa mtandao au kwa njia nyingine yoyote ya elektroniki. Tunatunza taarifa zako katika sehemu salama ikiwa ni pamoja na kompyuta, faili na rekodi zingine, na tunachukua hatua za kulinda taarifa zako binafsi dhidi ya utumiaji mbaya, upotezaji, ufikiaji usioidhinishwa, au kufichuliwa kwa mtu yeyote. Tunapofikiria kuwa taarifa zako binafsi hatuziitaji tena, tutaondoa maelezo yoyote ambayo yatakutambulisha.

2. Ni kwa namna gani tunatumia taarifa zako?

Taarifa tunazochukua kwako tunazitumia katika namna zifuatazo:

 1. kuthibitisha utambulisho wako na kuanzisha uhusiano wako na sisi
 2. kukupatia bidhaa na huduma zetu, au habari kuhusu bidhaa na huduma zetu kadiri ya mahitaji yako
 3. Kuomba ushauri ili kutusaidia kuboresha bidhaa na huduma zetu ili tuweze kukidhi maitaji yako
 4. kuunda maelezo mafupi juu yako ili tuweze kukuelewa na kutoa bidhaa na huduma bora zaidi tunazoweza
 5. Kutusaidia kuweza kukufikia ili kukujibu maswali na shida zako juu ya huduma au taarifa zetu
 6. Tunaweza kuhitaji kutunza taarifa zako binafsi kadiri ya mujibu wa sheia za nchi, agizo la korti au mchakato mwingine wa kisheria
 7. Kutunza rekodi za wateja (wanafunzi wetu) ili kuweza kuwafikia kirahisi kadiri ya mahitaji

3. Taarifa zako zipi Tunazohifadhi?

Taarifa zako binafsi tunazo hifadhi ni vile:

 1. Majina yako kamili
 2. Namba yako ya simu
 3. Barua pepe (email)
 4. Nakala ya kitambulisho chako

4. Uthibitisho wa Kukubali kuhifadhiwa na kutumia taarifa zako

Kwa kujiandikisha katika madarasa yetu ya Forex na Platforms zetu zote, unaashiria kukubali kwako na kuturuhusu kuhifadhi na kutumia taarifa zako. Ikiwa haukubaliani na sera hii ya taarifa binafsi, tafadhali usijiandikishe katika tovuti, madarasa au platform yetu yeyote ile.

NAKUBALIANA NA MASHARTI HAYA!.. NIPO TAYARI KUJIUNGA LEO