Create Account

Need some Help?

Tunakanusha mambo yafuatayo

Service Disclaimer

ScalpKingsFx ni kampuni inayojihusisha na biashara ya kubadili fedha za kigeni mtandaoni (online Forex Trading) pamoja na kutoa mafunzo ya jinsi ya kuifanya biashara hii kwa ufasaha (Forex Training). Mafunzo yote tunayoyatoa ni kwa madhumuni ya kielimu pekee na hayapaswi kuchukuliwa kama ushauri maalum wa uwekezaji katika masoko ya fedha au kuwa mbadala wa ushauri kutoka kwa mtaalamu wako wa maswala ya kifedha na uwekezaji. Wakufunzi (mentors) wetu wamechukua hatua stahiki kuhakikisha usahihi wa mafunzo yanayotolewa lakini Hakuna mkufunzi au mshauri kutoka ScalpKingsFx atakayewajibika kwa hasara yeyote utakayoipata kutokana na matumizi yeyote ya ushauri, elimu, ama taarifa nyingine yeyote iliyomo kwenye tovuti hii. Tumia tovuti hii na mafunzo yetu huku ukichukua tahadhari zako binafsi.

Create Account

Subscribe to our newsletters

3 Days Money Back Guarantee

Risk Disclaimer

Biashara ya kuuza na kununua fedha za kigeni mtandaoni inaweza kuwa fursa ngumu lakini pia yenye faida kubwa kwa wawekezaji. Kabla ya kuamua kushiriki katika soko la Forex, unapaswa kuzingatia kwa uangalifu malengo yako ya uwekezaji katika forex, kiwango chako cha uzoefu, na kiasi unachowekeza katika biashara hii. Muhimu zaidi, usiweke pesa ambazo huwezi kumudu kupoteza kwani kuna uwezekano mkubwa sana wa kupata hasara hata kupoteza kiasi chote katika ununuzi au uuzaji wa fedha za kigeni mtandaoni. Hivyo basi wakati wowote unaposhiriki katika masoko kama haya, unashauriwa kutumia kile kiasi cha fedha ambacho upo tayari kukipoteza.

Testimonial Disclaimer

Ushuhuda unaopatikana kwenye tovuti hii sio kiwakilishi cha matokeo ya wanafunzi au wateja wetu wote, wanafunzi na wateja wetu wengine wanaweza kuwa na matokeo mabaya zaidi kuliko ya hao walioonyeshwa kwenye ushuhuda. Ikumbukwe kuwa, Mafanikio ya mwanafunzi mmoja sio ishara ya matokeo au mafanikio ya wanafunzi wote. Watu waliotajwa na kuonekana katika ushuhuda uliotumiwa hawakulipwa kunukuliwa isipokuwa ni kwa matokeo yao ya ukweli. Matokeo yanatofautiana kati ya mtu na mtu na hakuna mwanafunzi anayehakikishiwa kupata faida au mafanikio katika biashara ya Forex.

Satisfaction Disclaimers

Ikiwa baada ya kumaliza mafunzo ya forex kutoka ScalpKingsFx, na kwa hali yoyote ukagundua kuwa haujaridhishwa na elimu iliyotolewa, unaweza kuomba kurudishiwa pesa ambazo umelipa na kama umelipia darasa letu lolote la mtandaoni ama huduma zetu nyingine tunazotoa mtandaoni unaweza kuomba kurudishiwa malipo yako ndani ya kipindi cha siku tatu baada ya kufanya malipo hayo. Pia ikiwa umenunua bidhaa yoyote inayotolewa na ScalpKingsFx kama vile programu, vitabu na machapisho mengine na ikatokea hujaridhika navyo, Mteja anastahili kuomba kurudishiwa malipo yake kwa muda wa week 1 tangu alipofanya manunuzi hayo.

BOFYA HAPA Kujaza fomu ya maombi ya kurudishiwa malipo

Trading Signals Disclaimers

ScalpKings Fx imekusanya best forex traders kuhakikisha wanatoa huduma bora ya biashara ya forex ikiwemo viashiria vya biashara (Trading Signals). Japo Viashiria hivyo vya biashara (Trading signals) vinavyotolewa na team nzima ya ScalpKingsFx havina uhakika wa 100%, na signal hizi hazitakiwi kuchukuliwa kama uhakika wa wewe kupata faida. Hasara yeyote inayoweza kujitokeza kutokana na kiashiria cha biashara kilichotolewa na ScalpKingsFx na ukakitumia kufungua biashara itakuwa juu yako mwenyewe na hakuna mtu kutoka ScalpKings Fx atakayewajibika na hasara hiyo.

Oops

Who Am I?

Need this Content?

Sorry...!

Vigezo na MashartiKwa kupitia tovuti hii na kurasa zetu zozote, unakubaliliana na Masharti haya ya Matumizi, sheria na kanuni zote zinazotumika. Hakikisha unasoma vigezo na masharti haya kwa umakini kabla ya kujiunga na huduma yetu yeyote. Na ikiwa haukubaliani na Vigezo au Masharti haya, haupaswi kutumia au kupitia tovuti hii au kurasa zetu zozote au kujiunga na huduma yetu yeyote ile.

1. Kibali cha Matumizi

ScalpKings Fx imetoa ruhusa kwa mtu yeyote kupakua/download nakala ya video au machapisho yeyote yanayoweza kupakuliwa kwenye tovutio hii kwa lengo la mtu kutazama au kujifunza binafsi na siyo kibiashara. Kibali hicho ni cha matumizi tu na sio uhamisho wa umiliki, na chini ya kibali hicho huruhusiwi kufanya mambo yafuatayo:

  1. Kunakili au kurekebisha maandishi, michoro, video, sauti, programu, au nembo zilizopo katika tovuti hii na bidhaa zetu
  2. kutumia maandishi, michoro, video au sauti zetu kwa madhumuni yoyote ya kibiashara, au kwa onyesho lolote la umma (la kibiashara au lisilo la kibiashara) bila hidhini yetu
  3. Kujaribu kuharibu au kubadili programu yoyote iliyomo kwenye tovuti hii
  4. Kundoa hakimiliki yoyote au nukuu nyingine za wamiliki kutoka kwenye machapisho yanayopatikana kwenye tovuti hii

Utafutiwaa kibali hiki endapo utakiuka yoyote ya masharti haya ya matumizi au kibali hiki kinaweza kusitishwa na Kampuni wakati wowote.

2. Usahihi wa Taarifa Zetu

ScalpKingsFx imechukua hatua stahiki kuhakikisha usahihi wa taarifa zilizo kwenye tovuti hii pamoja na mafunzo yetu yote. Ingawa, ScalpKings Fx haitoi dhamana ya hasara inayoweza kujitokeza kwa kutumia taarifa za kwenye tovuti hii pamoja na mafunzo yetu kiujumla. Taatifa na mafunzo yanayopatikana kwenye tovuti hii ni kwa madhumuni pekee ya kusaidia wafanyabiashara wa forex kufahamu na kufanya maamuzi huru ya uwekezaji katika soko la fedha. Kabla ya mtu kijihusisha na biashara hii ya mtandaoni anashauriwa kupata ushauri kutoka kwa mshauri wake wa maswala ya kifedha na uwekezaji. ScalpKingsFx pia haitoi dhamana wala kukuhakikishia kuwa matokeo utakayoyapata kutokana na mafunzo yetu na utumiaji wa tovuti pamoja na programu zetu yatakuwa sahihi kwa 100% , au kwamba ubora wa machapisho, video au huduma nyingine zinazotolewa na ScalpKings Fx zitakidhi matarajio yako katika biashara ya Forex.

3. Tovuti zilizounganishwa kwetu

ScalpKingsFx haijakagua tovuti zote zilizounganishwa nayo na haiwajibiki kwa taarifa zozote zinazopatikana kwenye tovuti yoyote iliyounganishwa. Kuunganishwa kwa tovuti nyingine isiyo ya kwetu haimaanishi kupitishwa kwa usahihi na uhakika wa taarifa za tovuti hizo. Hasara za matumizi ya tovuti yoyote iliyounganishwa na tovuti yetu ziko kwa mtumiaji mwenyewe.

4. Uthibitisho na Ukomo wa Matumizi

Katika muda wote utakaokua unatumia huduma zetu ulizojisajili nazo kupitia tovuti za ScalpKings Fx, unakubali na kuthibitisha kuzitumia kwa kufuata masharti yaliyopangwa. Pia ScalpKingsFx ina haki ya kuzuia matumizi yako juu ya huduma zetu wakati wowote na kwa sababu yoyote ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa masharati ya matumizi ya huduma hizo.

NAKUBALIANA NA MASHARTI HAYA!.. NIPO TAYARI KUJIUNGA LEO