Hii ni tutorial fupi inayoelezea maneno maarufu yanayotumika katika biashara ya forex kama mbadala wa yale yaliyozoeleka. Kitu cha msingi kabisa kwenye hii tutorial ni kuelewa maana na matumizi ya Ask price, bid price pamoja na Spread. Ask Price = Selling price/bei ya kuuzia kwa broker kwaiyo wewe ukitaka kununua hiyo fedha basi hiyo kwako itakuwa ndo Buying price/bei ya kununulia. Bid Price = Buying price/bei ya kununulia kwa broker hivyo basi wewe ukitaka kuuza hiyo ndo itakuwa bei yako ya kuuzia/selling price
Beginners Class Lectures
15
Tutorial hii inaelezea historia fupi ya biashara ya forex, namna inavyofanya kazi na kwanini inakuwa moja ya fursa ya kujitengenezea kipato mtandaoni. Pia, tutorial hii inaelezea vitu vya msingi ambavyo mtu anatakiwa kuwa navyo ili aweze kuanza biashara hii ya kubadilisha fedha za kigeni mtandaoni. Na mwisho kabisa inaelezea ni makundi yapi ambayo kwa namna moja au nyingine, kwakujua ama kwa kutokujua, yanajihusisha na biashara hii ya forex
Tutorial hii inakuelezea sababu za msingi za wewe kuamua kuchagua kufanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni mtandaoni badala ya kwenda kuwekeza pesa zako katika biashara nyinginezo. Mimi binafsi niliamua kufanya hii biashara kutokana na hizi sababu na sijawai kufikiria kuacha kuifanya japokuwa sio biashara pekee ninayofanya. Vile vile katika tutorial hii utapata kuzijua ni fedha zipi za kigeni ambazo zinabadilishwa mtandaoni maana sio kila fedha utaweza kuibadilisha mtandaoni, mfano Shilingi ya Tanzania, Kenya ama Uganda na utajua ni kwanini haiwezekani.
Tunafahamu kila biashara hua ina msimu wake, hata biashara hii ya kubadilisha fedha za kigeni ina kipindi chake pia japo ni tofauti na ukilinganisha na vipindi vya biashara nyingine yeyote ile unayoifahamu. Kipindi cha kufanya biashara ya forex ni masaa 24, jumatatu hadi ijumaa kwa mwaka mzima, japo kipindi hiki kimegawanyika katika masoko makuu manne. Katika tutorial hii utapata kujua aina kuu nne za masoko ya fedha (forex market sessions) na ni fursa zipi unazoweza kuzipata katika kila soko.
Kupata muda wa kila soko katika masaa ya nchi yeyote unayokuwa, tembelea hii wesite www.forex.timezoneconverter.com kisha kwenye Time Zone chagua Nchi na mji unaokuwepo
Katika tutorial hii utaenda kujifunza vitu vikuu vitatu ambavyo unatakiwa kuvielewa kiundani zaidi kabla hujaanza kuifanya biashara hii. Vitu hivyo ni Echange Rate, PIP pamoja na Lot Size. Kusingekuwa na mabadiliko ya viwango vya thamani kati ya fedha mbili basi kusingekuwa na fursa yeyote ya kujitengenezea kipato, pia unatakiwa ufahamu ni namna gani viwango hivyo vya thamani vinabadilika na ni jinsi gani ya kubadilisha viwango hivyo vya thamani kwenda kwenye faida hisika. Katika tutorial zote za darasa hili, hii ni sehemu muhimu sana na ninakushauri uifuatilie kwa umakini zaidi na kuhakikisha umeielewa kabla ya kuendelea na lectures zinazofuata.
Hii ni tutorial fupi inayoelezea nini maana na matumizi ya Leverage katika biashara ya forex. Kwa maana ya kawaida kabisa, Leverage ni matumizi ya hela ya mkopo katika kulipia uwekezaji fulani kwa makubaliano ya kuirejesha. Katika biashara ya forex, tunakopeshwa fedha na forex brokers ili kutuwezesha kununua kiasi kikubwa cha fedha za kigeni lakini fedha hizo HATUDAIWI wala KUZIRUDISHA (hii ni moja ya faida za kufanya biashara ya forex. Rejea Lecture ya 2 ). Sababu ya kutodaiwa wala kurudisha ni kwamba hasara zote tutakazopata zitakua ni zile tuu za pesa yetu tulowekeza na ikitokea tumepata hasara kiasi cha kumaliza uwekezaji wetu na kukaribia kupoteza zile fedha za mkopo basi hawa ma brokers huwa wanafunga hiyo biashara ili kuzilinda fedha zao.
Tutorial hii inaelezea terms ambazo siku zote unazofanya forex utakua unakutana nazo na kuzitumia. Maneno haya yanapatikana katika platform ambayo unaitumia wakati wa kufanya forex na kila neno linakuwa na maana yake pamoja na matumizi katika biashara ya forex. Watu wengi wamekuwa wakikimbilia kuingia sokoni na ku trade bila ya kufahamu vitu vya msingi kama hivi na matumizi yake kitu ambacho ni kosa kubwa sanaa.
Hii ni tutorial fupi inayoelezea maneno maarufu yanayotumika katika biashara ya forex kama mbadala wa yale yaliyozoeleka. Kitu cha msingi kabisa kwenye hii tutorial ni kuelewa maana na matumizi ya Ask price, bid price pamoja na Spread. Ask Price = Selling price/bei ya kuuzia kwa broker kwaiyo wewe ukitaka kununua hiyo fedha basi hiyo kwako itakuwa ndo Buying price/bei ya kununulia. Bid Price = Buying price/bei ya kununulia kwa broker hivyo basi wewe ukitaka kuuza hiyo ndo itakuwa bei yako ya kuuzia/selling price
Tutorial hii inaelezea namna mbali mbali za uingiaji sokoni. Unapoingia sokoni huwa tunasema ume "place order", hiyo order huwa inaambatana na conditions tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na unataka kununua au kuuza?, ni fedha ipi unayotaka kuinunua ua kuiuza?, ni kwa bei ipi unayotaka kununulia au kuuzia?. Unapokosea au kuchanganya kuweka aina fulani ya order basi unaweza ukajikuta order yako imekataliwa na broker ama unapata hasara ambayo hukuitegemea. Hivyo basi tumia muda katika kujifunza namna ya uingiuzaji wa order mbalimbali kabla hujaendela na mafunzo ya mbele zaidi
Tutorial hii inaelezea juu ya forex brokers, aina mbali mbali za hao brokers, jinsi ya ufanyaji kazi wa brokers, vitu vya msingi vya kuangaliwa wakati wa uchaguzi wa broker wa kutumia na mengine mengi kuhusu brokers. Ni vizuri wewe kama retail trader wa kwenye soko la fedha ukafahamu kuhusu forex brokers maana kwa namna yeyote ile huwezi kufanya biashara hii ya forex pasipo kupitia kwa hawa ma brokers.
Tutorial hii inaelezea hatua ambazo unatakiwa kuzifuata wakati unafungua akaunti ya kufanyia trades kwa broker ili kuhakikisha unaifungua na kui verify kwa ufasaha. Haijalishi ni broker gani unamtumia ila hatua hizi zinatakiwa kufuatwa kwa broker yeyote yule.
Lecture hii inaelezea step kwa step namna ya ku download MetaTrader 4 au MT4 pamoja na ku install kwenye computer inayotumia windows. Hakuna utofauti mkubwa sana kati ya meta trader 4 na meta trader 5 kwenye matumizi lakini nakushauri kutumia MT4 maana ndio platform ambayo inakuwa supported na brokers wengi wa forex.
Tutorial hii inaelezea namna ya ku install MetaTrader 4 kwenye Apple Computer. MetaTrader 4 ni application ambayo imetengenezwa kwaajili ya computer zinazotumia windows operating system hivyo basi ukitaka ifanye kazi kwenye computer yako ya apple kuna hatua ambazo nimeelezea za kufata. Kama njia hii ikishindwa kufanya kazi kwako, kuna njia ya pili nimeelezea kwenye Lecture 12B.
Tutorial hii inaelezea namna ya ku install MetaTrader 4 kwenye Apple Computer. MetaTrader 4 ni application ambayo imetengenezwa kwaajili ya computer zinazotumia windows operating system hivyo basi ukitaka ifanye kazi kwenye computer yako ya apple kuna hatua ambazo nimeelezea za kufuata. Kama njia hii ikishindwa kufanya kazi kwako, kuna njia ya pili nimeelezea kwenye Lecture 12A.
Tutorial hii inaelezea jinsi ya kutumia platform ambayo inatumika katika kufanya forex trading kwenye computer yako. Ni platform ambayo inakukutanisha wewe pamoja na broker wako. kwa lugha nyingine naweza kusema ni platform inayo ku link wewe na soko la fedha na kukuwezesha kufanya biashara ya forex. Unapaswa kujua namna ya kuitumia ili uweze kufanya biashara yako vizuri. Kama utakua na swali lolote juu ya matumizi ya platform hii maana ina vitu vingi sanaa na sijavielezea vyote, basi usisite kunitumia swali lako hapa chini.
Katika tutorial hii utajifunza namna ya kutumia MetaTrader 4 kwenye simu yako, ikiwa ni pamoja na jinsi ya ku login, ku set charts zako, ku place na ku close orders, ku add tools za kufanyia analysis n.k. Ni rahisi sana kutumia Mt4 kwenye simu kuliko kwenye computer japo kuna vitu vingi sana ambavyo vipo kwenye computer na havipo kwenye simu hivyo basi unapaswa pia kufahamu matumizi ya MT4 kwenye computer
Trainer Profile
Mussa Sabayo
Mentor | Signal Provider | Market Analyst